The Puppy Episode

"The Puppy Episode"
Sehemu ya Ellen

"Susan...I'm gay." Ellen Morgan anafunguka.
Sehemu ya. Msimu 4
Sehemu 22/23
Imetungwa na Ellen DeGeneres
Imeongozwa na Gil Junger
Tarehe halisi ya kurushwa Aprili 30, 1997 (1997-04-30)
Waigizaji wageni
Msimu 4 sehemu

Orodha ya sehemu za Ellen

"The Puppy Episode" ni kisa chenye sehemu mbili ya ucheshi mfululizo wa televisheni Ellen. Kisa hiki kimejikita zaidi katika kumwelezea muhusika mkuu Ellen Morgan katika kutambua kwake kama yeye ni mpenzi wa mahusiano ya jinsia moja na kufunguka kwake kwa hadhira. Ilikuwa kisa cha 22 na 23 katika mfululizo wa msimu wa nne. Kisa hiki kilitungwa na nyota wa mfululizo huu Bi. Ellen DeGeneres akiwa pamoja na Mark Driscoll, Tracy Newman, Dava Savel na Jonathan Stark na kuongozwa na Gil Junger. Kisa kilirushwa kwa mara ya kwanza kupitia kituo cha TV cha ABC mnamo tarehe 30 Aprili, 1997. Jina la kisa lilitumika kama jina la siri kwa ajili kufunguka kwa Ellen na kuweka ule usiri mkubwa kabisa wa kisa kizima.

DeGeneres alianza kujadiliana na ABC mnamo 1996 kumfanya Morgan ajitokeze kama ni mpenda mahusiano ya jinsia moja. Wakati majibu ya makubaliano yalivyotoka tu, DeGeneres alijikuta katika tafakuri nzito juu yake mwenyewe na hata uhusika wake wa kufunguka kama shoga. Pamoja na DeGeneres mwenyewe kuwa anagusiagusia juu ya uhusika wake katika kufunguka akiwa ndani ya TV na nje ya TV na ndani ya kipindi, duru zilithibitika pale kisa kilivyoenda kuzalishwa mnamo mwezi wa Machi 1997.

Licha ya vitisho kutoka kwa wadhamini na makundi ya kidini, "The Puppy Episode" ilipata mafanikio makubwa sana ya kitahakiki, ilishinda tuzo chungunzima na ikawa moja kati ya kitu kikubwa cha kitamaduni. Hata hivyo, DeGeneres na kipindi chake wakapondwa sana kwa kuwa "kishoga mno"; mfululizo ukaghairishwa baada ya msimu mmoja na mwigizaji mwalikwa Laura Dern na Ellen wote wakaingia katika misukosuko mizito ya kazi ya uigizaji.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne